MBINU ZA KUMTAMBUA MTU ASIYE MKWELI
MFAHAMU MTU AMBAYE HAJAWAHI KUSEMA UKWELI KWENYE MAISHA YAKE
Ndugu msomaji, napenda kutumia nafasi hii kukualika katika makala yetu ya leo ili tuweze kujifunza wote kwa pamoja yale mazuri niliyoweza kukuandalia siku hii ya leo. Karibu tusafiri pamoja hadi tamati ya somo letu la leo.
Dunia imekosa watu wanaoongea ukweli, dunia imekabiliwa na upungufu wa watu wanaoongea ukweli. Ukweli umekuwa ni bidhaa adimu kupatikana katika zama hizi. Ukweli unatafutwa kila kona lakini uongo unapatikana kila mahali. Uongo hauna thamani ndiyo maana unapatikana sana lakini ukweli ni thamani kwa sababu unafichwa. Ukweli huwa hauna huruma na mtu, ukweli huwa haumbembelezi mtu hata siku moja.
Rafiki, japo watu wanatumia kila mbinu kuficha ukweli lakini ukweli huwa haufichiki. Hata ukificha utajulikana tu, ukweli ni kama asili hivyo kwa mfano huwezi kulificha jua wakati linawaka mchana. Sasa rafiki yangu leo ninakushirikisha mtu ambaye hajawahi kuongea ukweli tangu azaliwe hapa duniani. Je unamjua ni mtu gani?
Ndugu msomaji, mtu ambaye hajawahi kuongea ukweli tangu azaliwe hapa duniani ni mtu ambaye ana hofu. Mtu mwenye hofu hajawahi kuongea ukeli hata siku moja katika maisha yake. Hofu inafisha ukweli wa vitu vingi hapa duniani. Watawala wanaongoza watu kwa kuwajaza hofu wale wanaowaongoza hivyo watu nao wanafanya kazi kwa hofu bila kuleta matokeo ya ukweli ndani yake.
Hofu haijawahi kusema ukweli. Mtu anayeongozwa na hofu anakuwa ni rafiki wa kudanganya tu. Hofu ni mwongo mkubwa sana katika maisha yetu. Anatudanganya vitu vingi sana katika maisha yetu. Hofu anachochoea watu wasiweze kuchukua hatua katika maisha yao. Hofu amekuwa ni adui wa kuua ndoto za watu wengi. Hofu amenyang’anya utajiri watu wengi duniani. Dunia inashindwa kuendelea kwa sababu ya watu kumkumbatia bwana hofu.
Kila kona ya maisha yetu hofu ndiyo iliyotawala ukilinganisha na ukweli. Watu wanalelewa katika misingi ya kujazwa hofu. Habari na jumbe za hofu katika mitandao ya kijamii lakini pia vyombo vya habari ndiyo vimetamalaki. Hofu inawafanya watu kuona dunia si sehemu salama ya kuishi. Hofu inawakatisha watu tamaa na kuona hakuna maana ya kuishi hapa duniani. Hofu amukuwa anaiba furaha za watu wengi na hatimaye na kuwaachia watu huzuni tele kwenye maisha yao.
Hatua ya kuchukua leo, utafute ukweli na upende ukweli. Tafuta ukweli wa kile kitu kinachokutia hofu sana. Kuwa balozi mzuri wa kutosambaza habari hasi zinazotia hofu maisha ya watu. Usiwe mvivu wa kukubali ukweli kwani ukweli ndiyo uhuru wa mtu. Usiruhu akili yako kusoma kitu ambacho ni hasi na kinaleta hofu wala masikio yako kusikia.
Mwisho, ujaja wa maisha ni kuujua ukweli na ujinga wa maisha ni kutoujua ukweli. Uvae ukweli ili uweze kuondoa ukungu wa hofu katika maisha yako. Simama imara kwani ukweli huwa unapingwa sana kwa kuusimamia lakini pia hata kusema pia. Kuwa na maisha ya uhuru kwa kuupenda na kuujua ukweli.
Rafiki, kupata vitabu vya mafundisho mazuri yatakayokupa mwongozo mzuri wa kuishi maisha ya furaha na mafanikio makubwa tafadhali BONYEZA HAPA au wasiliana nasi kupitia namba hizi tuweze kukuhudumia 0717101505/0767101505. Kujiunga na mfumo wetu wa kupokea makala kwa njia ya email tafadhali jiunge na kwa kujaza fomu hapo chini ya makala. karibu sana na asante sana.
No comments